Nicodemus Nyambane

Nicodemus Nyambane

Manati ya Kiswahili, Toleo la KCPE ni mwongozo thabiti kwa mwanafunzi na mwalimu katika maandalizi ya mtihani KCPE. Kina upekee na mbinu elekezi kutokana na jinsi kilivyopangwa kukabiliana na mtihani wa Kiswahili kwa njia rahisi. Kitabu hiki ndicho dira ya kumwelekeza mshikadau yeyote hasa katika utunzi wa mitihani nchini na katika jumuiya zote zinazoshabikia Kiswahili ulimwenguni. Viwango vyake vinalandana moja kwa moja na vile vinavyotumiwa katika utunzi na utahini nchini Kenya. Waandishi wa kitabu hiki, Tom Nyambeka na Nicodemus Nyambane, ni walimu waliobobea. Wana tajriba pana na uzoefu katika ufundishaji na utahini wa Kiswahili katika shule za msingi. Mbinu zilizotumiwa kwenye uwasilishaji wa kitabu hiki ndizo hizo waandishi wenyewe wamekuwa wakizitumia wakaibuka kwa alama maridhawa katika shule zao na taifa zima kwa jumla. Waandishi hawa wamejitahidi kuyaziba mapengo bayana katika Kiswahili na kuihakiki hiyo silabasi na kutuandalia ‘manati’ itakayowasaidia wanafunzi na walimu kupata lengo walilolikusudia.

Let's Connect

Books By Nicodemus Nyambane