Availability: In Stock

Manati Ya Kiswahili Toleo la Darasa la Saba

Author: Tom Nyambeka
ISBN: 978-9966-082-19-0

KSh700.00

– Mwongozo wenye ufafanuzi mwafaka wa namna ya kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa Kiswahili.
– Ufafanuzi na maelezo mapana ya hatua kwa hatua kuhusu vipengele vyote vya sarufi kwa mujibu wa silabasi ya sasa ya shule za msingi.
– Maelezo yakinifu kuhusu mbinu na utaratibu aula wa kusoma na kuelewa vifungu vya ufahamu na namna ya kujibu maswali yote yatokanayo na vifungu hivyo.

Description

Manati ya Kiswahili, Toleo la Darasa la Saba ni mwongozo thabiti kwa mwanafunzi na mwalimu katika maandalizi ya mtihani. Kina upekee na mbinu elekezi kwa wanafunzi na walimu kutokana na jinsi kilivyopangwa kukabiliana na mtihani wa Kiswahili kwa njia rahisi. Kitabu hiki ndicho dira ya kumwelekeza mshikadau yeyote hasa katika utunzi wa mitihani nchini na katika jumuiya zote zinazoshabikia Kiswahili ulimwenguni. Viwango vyake vinalandana moja kwa moja na vile vinavyotumiwa katika utunzi na utahini nchini Kenya. Mwandishi wa kitabu hiki, Tom Nyambeka ni mwalimu aliyebobea. Anayo tajriba pana na uzoefu katika ufundishaji na utahini wa Kiswahili katika shule za msingi. Mbinu zilizotumiwa kwenye uwasilishaji wa kitabu hiki ndizo hizo mwandishi mwenyewe amekuwa akizitumia akaibuka kwa alama maridhawa shuleni mwake na taifa zima kwa jumla. Mwandishi huyu amejitahidi kuyaziba mapengo bayana katika Kiswahili na kuihakiki hiyo silabasi na kutuandalia ‘manati’ itakayowasaidia wanafunzi na walimu kupata lengo walilolikusudia.

Baadhi ya yaliyomo ni:
– Mwongozo wenye ufafanuzi mwafaka wa namna ya kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa Kiswahili.
– Ufafanuzi na maelezo mapana ya hatua kwa hatua kuhusu vipengele vyote vya sarufi kwa mujibu wa silabasi ya sasa ya shule za msingi.
– Maelezo yakinifu kuhusu mbinu na utaratibu aula wa kusoma na kuelewa vifungu vya ufahamu na namna ya kujibu maswali yote yatokanayo na vifungu hivyo.

Additional information

Book Author

Year

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Manati Ya Kiswahili Toleo la Darasa la Saba”

Your email address will not be published. Required fields are marked *