Nsemia Inc. Publishers

“Wavuvi”  Riwaya Yenye Uhondo usio Haba

Riwaya ya Wavuvi yake Samuel Mwenda ni kati ya vitabu vyenye mvuto na uhalisia wa hali ya juu.  Kimejikita kwake Fadhila, mhusika mkuu. Ni matumaini yangu utakipenda na kupata kisa katika hali halisia. Masuala ya dini, ukatili chuki na mazingaombwe hayajaachwa nje katika Wavuvi.

Kisa kinaanza pale ambapo tunamwona Inspekta Macho akiwa mawazoni kuhusu visa vya kustusha vya kila mara. Watu wamekuwa wakiuwawa na kunyofolewa sehemu zao za siri. Hapa kitendawili ni je, atafanikiwa kuwanasa wanaohusika katika shughuli hii ya uhayawani na kwa njia zipi? Anashirikiana kwa ukaribu na Koplo June katika kuweka mikakati ya kuwanasa wahalifu hawa na kuwaweka vitabuni.

Mtindo unazidi kushika kasi pale ambapo tunampata mhusika mkuu Pasta Fadhila anapopiga hatua katika kuwavua watu. Fadhila alitoka familia iliyokuwa na shida si haba na vifo vya wazazi wake vikamwadhiri pakubwa. Anayo azma ya kuwa pasta na kuwavua watu. Swali ambalo hatuwachi kujiuliza ni je, safari yake katika uvuvi itakuwa nzuri ama itakumbwa na vizungumkuti? Vikwazo ni vipi na ni hatua zipi atakazotumia kuvikwepa na kuhakikisha yu imara katika misheni yake?

Yeye kama mtumishi wa Mungu, wafuasi wake hawamwoni kama mtu wa kawaida. Akiwa na sifa ya utu, alipiga hatua ya kutaka kumwoa mmoja wa washirika wake. Hata kama anafaulu, bado vikwazo vipo vingi katika ndoa yake. Habadili misimamo yake na bado imani yake haikutingika ikazidi kuwa imara. Jinsi anavyoepuka visiki kama si baraka basi ni miujiza ya nadra.

Mwishoni tunampata pasta Kanani anategemewa kuja na kuwaponya watu na kuwatoa katika njia za giza. Aliaminika sana kwa uponyaji wa hali ya juu kwa njia za maombi. Kisa kinakuwa kitamu sana katika kilele pale ambapo watu wanatupu na kukiri makosa yao hata wale ambao hatutarajii. Ilidhihirika kwamba safari ya kwenda mbinguni ni ya mtu binafsi na wala si umati. Hakika ni kitabu chenye msisimko mkubwa na chepesi kuelewa. Nakupendekeza usome Wavuvi na ukutafute katika maktaba ya vitabu iliyokaribu nawe ujipe uhondo.

Reviewed By:

Na Abel Nyamari

Nsemia Inc. Publishers

Nsemia Inc. Publishers

Leave a Reply

Shopping cart close