Availability: In Stock

Mama Panya na Mtoto wake Chepsoo

Author: Dorothy Jebet
ISBN: 978-9966-082-13-8

KSh250.00

Kitabu hiki kinafunza umuhimu wa tabia njema kwa watoto wadogo, na pia kuwafunza kuheshimu wazazi na wakubwa wao.

Description

Kitabu hiki kinafunza umuhimu wa tabia njema kwa watoto wadogo, na pia kuwafunza kuheshimu wazazi na wakubwa wao. Mwandishi, Dorothy Jebet, ana uzoefu wa miaka kumi na nane katika uandishi wa habari nchini Kenya. Amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali kama vile chombo cha habari cha Nation, Standard, Kenya Times, Star, na Kass FM katika nyadhifa mbalimbali. Kwa sasa, Dorothy ni mshauri wa kibinafsi kwa maswala ya uandishi wa habari.

Amejipatia mafunzo ya kina katika uandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ya kuripoti masuala ya Bunge la Marekani chini ya uongozi wa Bill Clinton. Kazi za Dorothy ni za kina, na baadhi yake zimevutia uangalifu wa kimataifa. Hadithi yake kuhusu ndoa ya mapema ya msichana mmoja mwenye miaka kumi na sita, ilimshindia udhamini wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) kusomea masomo ya Haki za Binadamu na Utawala katika Chuo Kikuu cha Lund.

Additional information

Book Author

Year

Price (U$)

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mama Panya na Mtoto wake Chepsoo”

Your email address will not be published. Required fields are marked *