Availability: In Stock

Manati ya Kiswahili Toleo la KCSE Lugha

KSh500.00

Kitabu hiki kimegawika katika sehemu nne muhimu. Hizi ni matumizi ya lugha, sifa/mifanyiko ya Kiswahili, isimu jamii, na historia ya Kiswahili. Mbali na maelezo murua kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na ufahamu na ufupisho, pana maelezo yaliyotolewa kwa utondoti kuhusu michakato ya matamshi na aina kadha wa kadha za maneno. Pameangazwa pia ngeli za Kiswahili kama zinavyotumika hivi leo na misingi ya maneno.

Description

Kitabu cha Kiswahili: Ufahamu na Ufasaha

Kitabu hiki kimegawika katika sehemu nne muhimu. Hizi ni matumizi ya lugha, sifa/mifanyiko ya Kiswahili, isimu jamii, na historia ya Kiswahili. Mbali na maelezo murua kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na ufahamu na ufupisho, pana maelezo yaliyotolewa kwa utondoti kuhusu michakato ya matamshi na aina kadha wa kadha za maneno. Pameangazwa pia ngeli za Kiswahili kama zinavyotumika hivi leo na misingi ya maneno.

Johari hii aidha imevinjari fani ya uakifishaji, kauli za usemi, na ukanushaji. Imemulika sintaksia ya Kiswahili katika mikabala tofauti tofauti na maneno yenye viambishi maalumu. Kwa umbuji unaostahiki, watunzi wamepiga darubini minyambuliko ya vitenzi na wakadadavua visawe, vitawe, na vitate.

Kitabu hiki vilevile kimewanda katika isimu jamii palipotaliiwa dhana, sajili, sifa, dhima ya lugha, na kadhalika ngazi za kutambulisha lugha. Isitoshe, kitabu hiki kimeshughulikia historia ya Kiswahili kuanzia chimbuko, maenezi, changamoto za maenezi, mchakato wa usanifishaji, na mustakabali wa Kiswahili.

Lugha iliyotumika katika kitabu hiki ni nyepesi suala ambalo litawezesha wanafunzi na walimu watakaotumia kitabu hiki kuelewa mada kwa wepesi bila mahitaji ya ufafanuzi wa kina.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Manati ya Kiswahili Toleo la KCSE Lugha”

Your email address will not be published. Required fields are marked *