Kitabu hiki kimegawika katika sehemu nne muhimu. Hizi ni matumizi ya lugha, sifa/mifanyiko ya Kiswahili, isimu jamii, na historia ya Kiswahili. Mbali na maelezo murua kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na ufahamu na ufupisho, pana maelezo yaliyotolewa kwa utondoti kuhusu michakato ya matamshi na aina kadha wa kadha za maneno. Pameangazwa pia ngeli za Kiswahili kama zinavyotumika hivi leo na misingi ya maneno.