Availability: In Stock

Chachu za Waja

ISBN: 978-9966-082-79-4

KSh850.00

Udhalimu wa wanawake na wanaume ni suala la kawaida. Kazi hii inadhihirisha uhalisia wa maisha katika familia nyingi za kisasa ambapo kuna ufeministi ambapo hata mwanamke anahisi kuwa nguzo ya familia. Maisha hayo ni sawa na yale watu waliyokuwa wakiishi katika nchi dhahania ya Sokoya, iliyokuwa na makabila mawili yaani Wakomoro na Warambi.

Category:

Description

Udhalimu wa wanawake na wanaume ni suala la kawaida. Kazi hii inadhihirisha uhalisia wa maisha katika familia nyingi za kisasa ambapo kuna ufeministi ambapo hata mwanamke anahisi kuwa nguzo ya familia. Maisha hayo ni sawa na yale watu waliyokuwa wakiishi katika nchi dhahania ya Sokoya, iliyokuwa na makabila mawili yaani Wakomoro na Warambi.
Riwaya yenyewe, inadhihirisha dhahiri shahiri jinsi wanaume wanavyodhulumiwa na wake zao. Bw. Mkata ni mfano bora anayedhalilishwa na mkewe Zekelina, mwanamke mashuhuri na maridadi katika mavazi yake kwa sababu ya hali yake ya uchechefu wa pesa. Latifu pia anadharauliwa na mchumba wake Firinda anayetambua kuwa hajatahiriwa kwa mujibu wa utamaduni wa Rambi.
“….ujue kwamba sikutaki tena nyumbani kwangu, muda wako uliisha zamani. Wewe kwa kweli si wa hadhi yangu.” Alisema Firinda akimfukuza Latifu. Latifu alilia akadondokwa na machozi mengi yaliyomlowa mwili mzima, na kutiririka hadi yakaunda kijito cha maji. “Kweli mapenzi uchizi! Kwa nini umekuja katika maisha yangu ili uniumize? Kwa nini umeruhusu moyo wangu akupende halafu uje kuniacha njiani? Ina maana wakati ulinishawishi nikupende hukuyajua haya…”

Kinyume na matarajio, mahusiano yanazuka wakati ambapo wanawake wanawapenda wanaume na kuvuka mipaka na kutangaza hisia zao. Peremina anamchumbia Isma naye Firinda anamsalitikia Latifu na mahusiano hayo mawili yanaishia kwenye machozi.

Maoni ya wasomaji…
Anuani “Chachu za waja” inaafiki matukio yaliyoangaziwa kwenye kazi yenyewe. Pengine hakuna anuani bora zaidi ya Chachu za waja kusawiri
dhamira ya mwandishi.
Mwandishi ametumia mbinu ya kipekee ya chachu katika harakatio za kuunda kazi yake kuonesha kwamba, swala analolizungumuzia lipo na
waathirika ni wengi.

Additional information

Book Author

Price (U$)

Year

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Chachu za Waja”

Your email address will not be published. Required fields are marked *