Availability: In Stock

Mashairi Teule

Author: Anisur Rahman
ISBN: 978-9966-082-75-6

KSh800.00

Ni vigumu kwa mtu kuelewa,
Kilicho muhimu zaidi kwa malenga-
Ni ushairi ama utu?
Ama ushairi ndio ubinadamu . . .

Category:

Description

Ushairi unafaa kulenga kuathiri nafsi ya binadamu, na si kuwa tu mpangilio wa maneno na sauti kwenye ukurasa. Haufai kuwa tu mchezo wa kuvutia kwa maneno, bali unafaa kukita mizizi kwenye mchanga ambapo umepandwa na kunawiri. Unafaa kuoana na ulimwengu wa masaibu ya binadamu, matumaini ya binadamu na kutamauka, na harakati ya kuyapa uzito hayo yote.Ushairi unafaa kuangazia shughuli za kibinadamu ili kutupatia maana halisi ya maisha yetu na sababu ya kuwepo.
Mkusanyiko wa Anisur Rahman ‘Mashairi Teule’ unahusiana na masuala ya kisiasa na kijamii, hususan Bangladesh ambapo mwandishi alizaliwa, na Uswidi ambapo anaishi, masuala yanayofanana na yale katika nchi yangu ya Kenya ninamoishi. Alivyoandika mwandishi huyu katika mojawapo ya mashairi yake, “Picha ya Malenga”, ushairi unafaa kuhusiana na ubinadamu:

Ni vigumu kwa mtu kuelewa,
Kilicho muhimu zaidi kwa malenga-
Ni ushairi ama utu?
Ama ushairi ndio ubinadamu . . .

Additional information

Book Author

Price (U$)

Year

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mashairi Teule”

Your email address will not be published. Required fields are marked *